The House of Favourite Newspapers

JPM: Bahi Nichagueni Niwaletee Maendeleo Zaidi – Video

0

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli amewaomba wananchi wa wilayani Bahi mkoani Dodoma, kumchagua ili awaletee maendeleo zaidi.

 

Ameyasema hayo leo wakati akindelea na kampeni za kuwania nafasi hiyo kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika  Oktoba 28, 2020.

 

“Sikutegemea kama ningekuta watu wengi hapa Bahi, leo nina mikutano mingi sana, ningependa sana nikae hapa kwa masaa mengi lakini nimeona maendeleo mliyonayo, miaka mitano iliyopita nilipita nikawaomba kura kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kweli.

 

“Nimeomba kura kwa sababu kubwa moja tu; kuwaletea maendelo ya kweli Watanzania. Hapa Bahi tumejenga shule, madarasa, tumetoa elimu bure, nimekuja kuomba kura ili nikaendelee kuyatekeleza ya elimu bure, siyo mwanafunzi anarudishwa nyumbani kisa ada, nataka hii burebure iendelee.

 

“Tumejenga Hospitali ya Wilaya ambayo ujenzi wake umefikia 95% kwa Tsh Bilioni 1.8, nataka hii Hospitali ya Wilaya imalizike haraka ili wananchi wa Bahi wawe wanatibiwa hapahapa na ndiyo maana ninawaomba mnipe kura nikamalizie kiporo kilichobaki.

 

“Tumeleta umeme vijiji vyote, ninajua kuna vijiji 16 tu vya wilaya hii ya Bahi havijakamilisha umeme, nipeni miaka mingine mitano nikamalizie kabisa, sitawaangusha.

 

“Kwenye miaka 5 tutaendeleza jitihada kwa kukamilisha pale tulipoishia, tutaendelea na ujenzi wa vituo vingine vya afya, tutaendelea kuboresha elimu bila malipo, tutahakikisha tunafikisha umeme kwenye Vijiji 16 vilivyobaki kwenye Wilaya hii ya Bahi.

 

“Sasa hivi Makao Makuu ya Nchi yetu yapo Dodoma na mimi mwenyewe ninakaa Dodoma, sitashindwa kufanya maendeleo katika Wilaya ya Bahi kwa sababu Bahi na Dodoma ni pua na mdomo,nawahakikishia sitawaangusha, tumetoka mbali.

 

“Nchi yetu ni miongoni mwa nchi 10 zenye maendeleo ya juu Afrika, katika ripoti ya mwaka 2020 nchi yetu ya Tanzania inaongoza kuwa mahali penye amani kwa Afrika Mashariki na katika Afrika nzima sisi ni wa 6 na katika Dunia nzima sisi ni wa 52.

 

 

“Siku ya uchaguzi Oktoba 28, naomba mnipigie kura, msisahau jina la John Pombe Joseph Magufuli.  Mtasahau jamani? Mpigie kura Magufuli tumalize hapohapo,” amsema Magufuli.

 

Leave A Reply