The House of Favourite Newspapers

Wanne Washikiliwa Na Polisi kwa Mauaji Na Kutelekeza Mwili Wa Marehemu-Video

0

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kumuua mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Elizabeth Bernard mwenye umri wa miaka 63 kisha kisha kutelekeza mwili wa marehemu mtoni.

 

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema tukio hilo lilitokea Septemba 10, 2021 majira ya usiku ambapo mwanamke huyo mkazi wa Himo Darajani aliuawa na watu watatu ambao majina yao yamehifadhiwa.

 

Mchunga mbuzi ambaye alikuwa akifanya kazi kwa marehemu huyo amekiri kufanya tukio hilo la kumuua boss wake akishirikiana na wenzake wa 3 na kutelekeza mwili wa marehemu mtoni.

 

Taarifa hiyo imetolewa na mfanyakazi wa ndani wa marehemu katika kituo cha polisi na mara moja msako ulianza na kubainisha watuhumiwa hao, na wakati wowote watafikishwa mahakamani kwa shtaka la uaji dhidi yao.

 

Aidha katika ripoti hiyo iliyosomwa na kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro ameishauri jamii yakua kabla haujaajiri mtu ni vizuri kujua historia yake na  kufanya hivyo itapunguza vifo majumbani

 

Leave A Reply