The House of Favourite Newspapers

Wapinzani Wa Yanga Waingia Mchecheto Mchezo wa Marudiano kwa Mkapa

0
Kikosi cha Yanga.

YANGA washindwe wenyewe kwani wapinzani wao, Rivers United wanatarajiwa kuwakosa wachezaji wao wawili tegemeo watakapokutana katika mchezo wa marudiano wikiendi hii utakaochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza ambao ulichezwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Godswill uliopo katika Mji wa Uyo, Nigeria, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 0-2 yaliyofungwa na Fiston Mayele.

Yanga inahitaji sare au ushindi wa aina yoyote dhidi ya Rivers United ili kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Rivers United, timu hiyo itamkosa beki wa kushoto, Ebube Duru na kiungo mshambuliaji, Williams Ukeme.

Rivers United

Mtandao huo ulisema pia upo uwezekano wa timu hiyo, ukamkosa mshambuliaji wao tegemeo, Paul Acquah ambaye alikosekana katika mchezo uliopita kutokana na majeraha yanayomsumbua.

Mshambuliaji huyo bado hajaanza mazoezi na wenzake, hadi wakati wakiwa katika maandalizi ya kuja Tanzania kucheza dhidi ya Yanga.

“Wakati timu ikijiandaa na safari ya kuja Tanzania kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga, huenda tukawakosa wachezaji wetu muhimu wawili hadi watatu.

“Wachezaji wote hao wana majeraha, Ebube na Ukeme walipata majeraha katika mchezo dhidi ya Yanga.

“Acquah alipata majeraha katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo ni pigo kwetu kuelekea mchezo huo wa marudiano dhidi ya Yanga,” ilisema taarifa hiyo.

STORI NA WILBERT MOLANDI

KIJANA ALIYEBUNI HELKOPTA SONGWE APEWA MIL 99 NA SERIKALI, AFUNGUKA ALIVYOPATA WAZO…

Leave A Reply