The House of Favourite Newspapers

Msafara Wa Viongozi Wa Chadema Wapata Ajali, Watano Wajeruhiwa – Video

0

Viongozi kadhaa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo, April 27, 2023.

Msafara huo ulikuwa ukielekea Kigoma kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa oparesheni mpya ya chama hicho.

Ajali hiyo imetokea Wilaya ya Uyui Tabora, Kata ya Kigwa ambapo waliopata ajali ni Yohana Kaunya Kaimu Katibu Mkuu Bavicha, Nuru Ndosi, Naibu Katibu Mkuu Bawacha Bara, David Chiduo, Josephat Magambo na Dereva Daniel Marwa.

Majeruhi wa ajali wanapatiwa matibabu katika Zahanati ya Kigwa B wilayani Uyui.

 

Leave A Reply