Wasanii Walivyojipanga Kuadhimisha Siku Ya Kimataifa Ya Kuigiza Jukwaani
Dar es Salaam 27 Machi 2024: Ikiwa leo Macho 27 ni Siku ya Kimataifa ya Maonesho ya Sanaa ya Kuigiza jukwaani na filamu Wadau wa sanaa nchini kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu wameelezea jinsi walivyojipanga kuadhimisha Siku ya Kimataifa kwa progam maalum iitwayo TAMBA NA JUKWAA.
Akizungumza na wanahabari leo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dk. Kiagho Kilonzo amesema bodi hiyo ambayo jukumu lake siyo filamu peke yake isipokuwa mpaka maonesho ya jukwaani mwaka huu wamejipanga kuadhimisha siku hiyo kwa matukio kadhaa yatakayokwenda na program iitwayo Tamba na Jukwaa.
Dk. Kilonzo amesema program ya TAMBA NA JUKWAA itahusisha maigizo mawili ambapo Machi 29 kutakuwa na igizo la pasaka katika eneo la Kanisa la KKKT Ubungo Dar na kufuatiwa na onesho la Aprili 20 mwaka huu liitwalo JUKWAA LA MTAA. litakaloongozwa na Ayubu Kondo Bongwe maarufu kama Black Jesus.
HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL