The House of Favourite Newspapers

WASHINDI WA DROO YA TISA NA KUMI WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

Rashid Simba (kulia) akikabidhiwa kadi na funguo za pikipiki na Sifael Paul, Mhariri wa Ijumaa Wikienda.

Washindi wa droo ya tisa na kumi wa Shindano la Tusua Maisha na Global, wamekabidhiwa zawadi zao, tukio ambalo limefanyika katika Ofisi za Global Publishers LTD, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

 

Waliokabidhiwa zawadi ni Rashid Simba na Ramadhan Mohamed waliojishindia pikipiki mpya kila mmoja, Geofrey John aliyekabidhiwa dinner set na Justus Rugambwa aliyekabidhiwa jezi.

Ramadhan Mohamed (kulia), akikabidhiwa kadi na funguo za pikipiki na Jimmy Haroub, Afisa Masoko wa Global Publishers.

Wengine ambao watatumiwa zawadi mahali walipo, ni Anna Mbise, mkazi wa Arusha aliyejishindia dinner set na Abdallah Benard aliyejishindia jezi.

Kutoka kulia, washindi Geofrey John, Justus Rugambwa, Rashid Simba na Ramadhan Mohamed wakiwa katika picha ya pamoja.

Wakati huohuo, washindi wa droo ya kumi na moja ambao ni Bolen Kilimba aliyejishindia pikipiki, Silvanus Nyombe wa Mwanza aliyejishindia dinner set na Eliuter Ndunguru wa Manyoni, Singida, wao watakabidhiwa zawadi zao sambamba na washindi wa droo ya mwisho inayotarajiwa kuchezeshwa Jumanne ya wiki ijayo, hivyo kuhitimisha safari ya kujishindia zawadi kedekede iliyodumu kwa muda wa wiki 12.

Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Global Publishers.

Ili kushiriki kwenye ‘penalti ya mwisho’, nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra.

Ramadhan Mohamed akiwa kwenye pikipiki yake.

Ukishanunua, funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.

Justus Rugambwa (kushoto) akipokea jezi kutoka kwa Judith Mlwale, mtangazaji wa Global TV.

Itume namba maalumu inayoonekana juu ya kuponi kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kuponi au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukulia zawadi.

Ramadhan Mohamed akikabidhiwa zawadi ya dinner set na Gasper Oiso.

 

 

Comments are closed.