The House of Favourite Newspapers

Wasanii Na Filamu Zilizoingia Kwenye Tuzo Za 2023 Watajwa, Msigwa Atia Neno Kwa Mastaa

0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa akizungumza kwenye mkutano huo.

Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo kupitia Bodi ya Filamu nchini imetangaza washiriki wa tuzo za filamu mwaka huu 2023 ambazo zinatarajiwa kufanyika Jijini Dar,  Desemba 16 mwaka huu.

Bodi ya Filamu imetangaza wasanii na filamu zilizoingia kwenye kinyanganyiroi cha tuzo hizo kwenye mkutano uliofanyika Hotel ya Four Points By Shereaton (zamani New Africa) jijini.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Bodi ya Filamu Dk. Kiagho Kilonzo amewaasa wasanii kutengeneza kazi zenye ubora zaidi kwa ajili ya kujiongezea thamani ya kazi yao kwakuwa sasa hivi sanaa ni kazi.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Bodi ya Filamu Dk. Kiagho Kilonzo kwenye hafla hiyo.

Kuhusiana na tuzo hizo amewaambia zitapigwa kwa mfumo kwa kisasa kabisa na kuwapa nafasi wenye simu za smart, hata ‘kitochi’ na laptop zenye data zitaweza kupiga kura kwenye kipengere husika.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa amesema anachotaka ni kuona Watanzania wanapata furaha kupitia sanaa ya filamu hivyo kwa upande atahakikisha sanaa hiyo inakuwa juu.

Msanii Single Mtambalike a.k.a Rich na wasanii wenzake wakitoa shukrani kwa wadhamini wa tuzo hizo.

Msigwa aliwataka mastaa wa filamu kuzidi kuipambania tasnia hiyo kwakuwa katika tuzo hizi hawataangalia ustaa bali ni uwezo wa kazi unavyoonekana katika kufurahisha jamii. Aliendelea kusema;

Joti na Chuchu Hans wakifuatilia matukio kwenye hafla hiyo.

“Nataka Tanzania furaha ya sanii ya filamu ichemke, Watanzania wanataka burudani, Watanzania wanataka ajira, Watanzania wanataka uchumi hivyo basi maelewkezo yangu kwa taasisi zote zilizopo chini ya wizara hii ni kwamba sitaki shughuli ndogo, hivyo katika tuzo hizi nazo sitaki ziwe za kibabaishaji.” Alisema Msigwa.

Msanii Batuli (kushoto) na Davina wakifurahia wakati wakisikiliza majina ya filamu na wasanii walioingizwa kwenye tuzo hizo.

Hafla hiyo ya kutangaza filamu na wasanii walioingizwa kwenye kinyang’anyiro hicho mastaa mbalimbali wa filamu nchini walihudhuria akiwemo, Single Mtambalike maarufu Rich, Halima Yahaya ‘Davina’ Batuli, Msanii maarufu wa vichekesho Joti na wengineo. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply