The House of Favourite Newspapers

Watatu Wafikishwa Kisutu Wakikabiliwa na Mashtaka Saba

0

Washtakiwa watatu wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka saba, yakiwemo ya kushiriki vikao vya kutengeneza mikakati ya ugaidi; kukutwa na vilipuzi na silaha pamoja na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania( JWTZ).

 

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka yao na Mawakili watatu wa upande wa mashtaka, wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Shadrak Kimaro akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon na Tulimanywa Majigo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

 

Washtakiwa wao ni Adam Kasekwa, Halufa Hassan maarufu kama Adamo na Mohamed Lingwenya, ambapo kwa pamoja wamesomewa kesi ya uhujumu uchumu namba 63/2020 chini ya sheria ya usalama wa taifa na sheria ya kuzuia makosa ya ugaidi.

 

Katika maelezo ya makosa hayo washatakiwa hao wanatuhumiwa kutenda makosa katika maeneo mbalimbali na ndani ya mikoa ya Dar es salaam, Arusha na Morogoro

 

Wankyo amesema kati Mei Mosi na Agosti Mosi mwaka huu watuhumiwa hao walishiriki kufanya makosa hayo.

Ameongeza kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kukutwa na vilipuzi pia wanatuhumiwa kula njama za kutaka kulipua vituo vya mafuta jambo ambalo linahatarisha usalama wa nchi.

 

Vile vile watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa ya kusafirisha madawa ya kulevya aina ya heroin.

 

Watuhumiwa hao hawakupaswa kujibu chochote kwani baadhi ya makosa yanayowakabili ni ya uhujumu uchumi na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 2, 2020 na upeleezi bado haujakamilika.

Leave A Reply