The House of Favourite Newspapers

Wasio na KONEKSHENI’ hawajaona ila imetosha!

KUNA matukio ambayo siku za hivi karibuni yametokea kwenye ulimwengu wa maisha ya mastaa Bongo na kushitusha sana. Nazungumzia matukio ya kuvuja mitandaoni kwa video za mastaa wakiwa na wapenzi wao faragha. Kama utakuwa umesahau nikukumbushe tu tukio la yule mwanadada Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ ambaye video yake ilimuonesha akiwa kimahaba na msanii mwenzake William Nicholaus Lymo ‘Billnass.

Sakata lao likawatesa sana hadi Baraza la Sanaa la Taifa likaingilia kati. Hatujakaa sawa mara ukatua ‘mzigo’ mwingine wa msanii wa muziki Rutyfiya Aboubakary ‘Amber Ruth’ akiwa na mpenzi wake Said Bakary Kitomali  wakifanya uchafu usioelezeka. Nao msala wao ukawasumbua sana hadi soo likatinga mahakamani.

Wakati soo la Amber Ruth likiwa bado la moto, tukashuhudia zikimwagika tena video za staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu naye akiwa na aliyekuwa mpenzi wake, PCK wakiwa kwenye ulimwengu wa mahaba motomoto. Naye msala ukamtikisa ile mbaya, akapelekwa mahakamani, akasota sana. Wakati matukio hayo yakiongozana, wadau wakaelezea jinsi mahusiano mengi yalivyo hatarini. Wakaeleza kuwa,

kama wapenzi wanaweza kufikia hatua ya kupigana video chafu kama hizo kisha kusambaa, basi mapenzi yameingiliwa na shetani. Maelezo hayo yalitosha kabisa kuwazindua wale walio kwenye  uhusiano, kwamba kwa hali ilivyo hakuna wa kumuamini pale unapokuwa faragha.

Hata kama ni mumeo au mkeo, ukishavua nguo zako iwe unabadili au labda mnaingia kwenye ‘majamboz’, hakikisha mpenzi wako hashiki simu maana hashindwi kutaka kuweka kumbukumbu kwa kukufotoa picha kisha zikaja kukuletea majanga. Cha ajabu sasa licha ya baadhi ya mastaa kukumbwa na misala mizito kwa video zao chafu kuvuja, bado kuna wengine hawajastuka.

Ndiyo maana juzikati tena likaibuka hili la msanii wa muziki ambaye pia ni MC, Menina Atick. Zikavuja video zake ambazo licha ya kwamba kilichokuwa kikifanyika si cha ajabu sana kwa wapenzi wanapokuwa kwenye ‘kuta nne’, lakini kwa kuvuja kwake

imekuwa ni aibu kubwa kwake. Sijajua hatima ya tukio lake hasa kufuatia serikali kuingilia kati huku pia wengi wakimtetea na kutakaaliyemrekodi kisha kuvujisha achukuliwe hatua kali. Niseme tu kwamba, matukio hayo ya video za mastaa kuvuja tena watu wao wa karibu wakitajwa kuhusika, ndiyo yaliyonifanya niandike makala haya. Naizungumzia hii tabia ya baadhi ya wapenzi wanapokuwa faragha kupigana picha za utupu! Hakika hili linanishangaza sana na nahisi wanaofanya hivyo hawana akili timamu.

Huwa najiuliza, mwanaume au mwanamke anapochukua simu au kamera kisha kumpiga au kumrekodi mpenzi wake akiwa kama alivyozaliwa ni ili iweje? Anazipiga kwa ajili ya matumizi gani? Ni swali ambalo hata wewe mwenye akili timamu unaweza kuwa unajiuliza na usipate majibu kwa haraka. Katika kujua kilicho nyuma ya pazia, nilijaribu kuzungumza na baadhi ya wanaume ambao ndiyo wanaotajwa sana kufanya kamchezo haka. Wapo waliosema wanafanya hivyo kwa kujifurahisha tu lakini wengine wakasema eti, ili wanapokuwa mbali na wapenzi wao wapate kitu cha kujiliwazia.

Si wanaume tu wanaosema hivyo, hata baadhi ya wanawake nao walisema hivyohivyo. Lakini sasa cha ajabu wapo waliokuwa wawazi zaidi kwa kusema kuwa, wanawapiga picha wapenzi wao wakiwa watupu ili wakigombana wazitumie kuwakomoa. Yaani mwanaume anampiga picha mpenzi wake ili siku wakikorofishana au akitaka kuachwa, aziachie kwenye mitandao ili kumkomoa. Sasa, ukiacha zile sababu nyingine, tusimamie hii ya kwamba wengi wanazipiga ili wakigombana na wapenzi wao wawaaibishe.

Wewe ambaye una akili zako timamu unakubalije sasa kupozi mbele ya kamera na kumruhusu mpenzi wako akufotoe? Hebu tuache huu ulimbukeni. Kupigana picha tukiwa watupu ni kinyume na maadili na sheria za nchi. Ukiona mpenzi wako anachukua simu yake kisha kutaka kukupiga, chukulia huyo hakupendi na siku hiyo iwe ndiyo mwisho wa uhusiano wenu.

Ninachokushauri wewe msomaji wangu uliye kwenye uhusiano ni kwamba, ukiwa faragha na mpenzi wako hata kama unampenda sana na unamuamini sana, kuwa makini naye. Sasa hivi kwa teknolojia ilivyo, watu wanapiga picha kwa siri kiasi kwamba ukizubaa utashangaa siku unaambiwa picha zako za utupu zipo, unabisha kumbe umepigwa na mpenzi wako bila wewe kujua.

Huwezi kuamini wapo watu kwenye ndoa lakini ukipekua simu zao wana picha za wake au waume zao wakiwa watupu, sasa kwa wapenzi wa kawaida hali ikoje? Lakini niwaase wale wenye ulimbukeni wa kujipiga picha wenyewe wakiwa watupu. Unakuta mtu yuko mbali na mpenzi wake, anaambiwa; baby nimekumis sana nitumie picha yako ukiwa mtupu’, bila kufikiria mara mbilimbili anapozi na kujipiga kisha anamtumia mtu ambaye wala hana uhakika wa kudumu naye.

Huu si ujinga jamani? Nihitimishe kwa kusema kwamba, huu utandawazi usituharibie maisha yetu. Tumeshaona wengi wakiingia matatizoni kwa kupigwa ama kujipiga picha wakiwa watupu, ni wakati wako wa kushtuka ili na wewe yasije yakakukuta. Najua kwa wasio na koneksheni hawakuona video za mastaa hawa, lakini niseme tu kwamba sisi wenye koneksheni tumechoka kuona upuuzi huo

MAKALA: AMRAN KAIMA

Comments are closed.