The House of Favourite Newspapers

Wasomaji: Hatujawahi kulikosa Betika

GAZETI la BETIKA, limeendelea kuwashika wasomaji kila kona kutokana na utofauti ilionao huku likitolewa burekwa watu wenye umri kuanzia miaka 18.

Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, linaingia mtaani kila Jumatano ambapo likiingia mtaani, timu ya maofisa masoko ya kampuni hiyo kutembelea mitaa mbalimbali.

 

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi tofauti duniani.

Leo Jumatano, timu hiyo ya maofisa masoko ilitembelea Kariakoo jijini Dar es Salaam na kukutana na wasomaji mbalimbali wa Gazeti la Betika.

Miongoni mwa wasomaji hao aliyejitambulisha kwa jina la Michael George, alisema: “Kila gazeti likitoka huwa natafuta nakala yangu, sipo tayari kuona nakosa na hapa wote huwa hatulikosi gazeti hili.

 

“Hili ni gazeti la bure, linawahusu watu wazima kuanzia umri wa miaka 18, linatolewa bure kabisa kwa wauza magazeti wote nchini.

“Wanaohitaji kutangaza nasi tunapatikana kupitia namba 0755826488 na 0712595636 au barua pepe[email protected], bei zetu ni nafuu, muhusika anaweza kufika Sinza Mori, Dar, kwenye jengo letu la Global Group.

 

“Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao yetu ya kijamii katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

“Kupitia hayo matangazo ambayo yapo ndani ya Betika, msomaji akijipatia nakala yake anapata faida mara mbili, kwanza kufahamu odds mbalimbali za kubet, lakini pia kufahamu mambo mbalimbali yanayowahusu watangazaji wetu hao,” alisema.

 

“Nafahamu linahusika na masuala ya kubeti na ukiangalia hivi sasa ligi zinaenda kuanza, hivyo itakuwa rahisi kubeti hasa kupitia gazeti hili.”

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema heshima ya Betika imeendelea kukua kila siku na sasa wanajivunia kuwa na idadi kubwa ya makampuni yanayotangaza biashara zao kupitia gazeti hilo hasa kwa kuwa bei yao ni nafuu na imewavutia wengi, huku akiongeza kuwa bado wanawakaribisha watu binafsi na makampuni kuleta matangazo yao.

Comments are closed.