The House of Favourite Newspapers

Wasomaji Kigamboni Dar wachangamkia droo ya pili ‘Shinda Nyumba’

0

2

Ofisa Masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda (katikati) akiwavalisha kofia wasomaji wa Gazeti la Uwazi wa eneo la Kigamboni Feri jana Februari 9 mwaka huu.

4

Msomaji wa Gazeti la Uwazi (kulia) wa eneo la Feri akiweka kuponi yake kwenye ndoo maalum ili kushiriki droo ya pili.

5

Wasomaji wa Gazeti la Uwazi wa eneo la Feri wakikata kuponi ili kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba inayotarajiwa kuchezeshwa hivi karibuni.

6

Zoezi la kuweka kuponi kwenye ndoo maalum ya kuponi za Bahati nasibu likifanyika eneo la Feri.

7

Wasomaji wa Gazeti la Uwazi wa eneo la Kigamboni Feri wakijaza kuponi.

8

Wasomaji wa Gazeti la Uwazi wakiwa wamependeza na kofia zilizo na nembo ya Shinda Nyumba.

9

Wasomaji wa Gazeti la Uwazi wakinunua gazeti hilo kutoka kwa muuzaji wa magazeti ya Global (aliyepo katikati mwenye fulana nyeupe)

11

Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda (kulia) akifuatilia namna msomaji alivyokuwa akijaza kuponi yake ili kushiriki droo ya pili.

12

Wasomaji wa Uwazi wakinunua gazeti kwa muuzaji ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

13

Uwekaji kuponi kwa wasomaji wa gazeti la Uwazi eneo la Feri ukiendelea.

14

Kuponi ikikatwa ili kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba.

15

Wadau wa gazeti la Uwazi wakiweka kuponi zao kwenye ndoo.

16

Wasomaji wa eneo la Mji Mwema Kigamboni wakinunua gazeti kwa muuzaji (mwenye fulana nyeupe katikati) ili kukata kuponi.

17

Wasomaji wa Gazeti la Uwazi wakiwa katika harakati za kukata kuponi zao ili kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba eneo la Mji Mwema.

WASOMAJI mbalimbali wa magazeti ya Kampuni ya Global Publishers inayochapisha magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi, Jumanne ya jana walionekana kuchangamkia droo ya pili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kwa wakazi wa Kigamboni jijini Dar kwa kujaza kuponi na kushiriki.

Maofisa masoko wa Global,Yohana Mkanda na Jimy Haroub walitembelea maeneo ya Feri,Mji Mwema, Ungindoni na Maweni kugawa zawadi za kofia zenye nembo ya Shinda Nyumba zilizokuwa zikitolewa baada ya kuwakuta wasomaji wakinunua gazeti la Uwazi linalotoka kila Jumanne.

Akizungumza na wakazi wa maeneo ya Kigamboni, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, alisema wasomaji wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kununua magazeti hayo na kukata kuponi ili kujinyakulia zawadi nyingi kwenye droo ya pili ya Shinda Nyumba itakayofanyika hivi karibuni, sambamba na kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi ya nyumba iliyopo eneo la Salasala jijini Dar katika droo ya mwisho.

“Global tumekwishatoa zawadi mbalimbali kwa wasomaji wetu kama vile, fulana, kofia, simu za kisasa, runinga na ving’amuzi vya TING katika droo yetu ya kwanza.
“Niwasihi watu wazidi kununua magazeti yetu na kujaza kuponi ili waweze kushiriki bahati nasibu yetu. Kitu cha muhimu kuzingatia, wawe na umri wa zaidi ya miaka 18,” alisema Mkanda.

(HABARI/PICHA; DENIS MTIMA/GPL)

Leave A Reply