The House of Favourite Newspapers

WASOMAJI SASA WAANZA KULIGOMBEA ‘BETIKA’

 

GAZETI la Betika ambalo ni maalum kwa ajili ya wapenzi wa burudani na wazee wa kubeti, leo Jumatano lilizidi kubamba kitaani na kugombewa na wasomaji walioanza kulielewa baada ya kikosi kazi ya usambazaji na masoko cha Magazeti ya Global Publishers watoaji wa gazeti hili, kuingia mitaani na kulisambaza bure kwa wapenzi wa burudani na kubeti.

Kikosi hicho kilitembelea baadhi ya maeneo maeneo ya Kimara Korogwe, Baruti, Temboni, Stop Over na Mbezi Mwisho ambapo mashabiki waliowahi kulisoma gazeti hilo siku zilizopita walionekana kuligombea kutokana na kuujua uhondo uliomo ndani yake.

Baadhi ya wasomaji  hao walisema walikuwa wakilisubiri gazeti hilo kwa hamu ili kufuatilia mambo mbalimbali yaliyomo kwenye gazeti hilo ambapo pamoja na kujua jinsi ya kubeti kiufasaha kuna habari mbalimbali za michezo ikiwemo ratiba za ligi mbalimbali misimamo, matangazo mbalimbali na mambo mengine.

Kwa wapenzi wa hadithi za kusisimua kuna hadithi ya Pendo ambayo imeonekana kuwashika wasomaji wengi ambao walisema hawataki kuikosa kila linapotoka gazeti hili.

Betika limeanza kujizolea umaarufu mkubwa kila kukicha huku likiendelea kugawiwa bure kwa wasomaji wenye umri za kuanzia miaka 18.    

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS

Comments are closed.