The House of Favourite Newspapers

Wasomaji Spoti Xtra Wachangamkia Ndinga ya ‘Baba Lao’

0
Afisa Masoko na Usambazaji, wa Global Publishers, Anthony Adam (Wa pili kushoto waliokaa) akiwaelekeza jinsi ya kushiriki shindano hilo wasomaji wa eneo la Tazara, Dar.

GARI  la wasomaji wa Championi na Spoti Xtra hilooo… Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia gari hilo kumpata mwenyewe Julai mosi mwaka huu.

Shindano hilo ambalo liliendeshwa kwa miezi kadhaa kwa wasomaji hao kushiriki bahati nasibu, hatimaye mshindi anatarajiwa kuondoka na gari hilo jipya aina ya Toyota Fun Cargo enye thamani ya shilingi milioni kumi.

Watani wa jadi, Simba na Yanga, wakitaniana wakati wakipata uhondo wa burudani ndani ya Spoti Xtra walipokutwa eneo la Buguruni.

Kitengo cha Masoko na Usambazaji cha magazeti hayo, leo Juni 25, 2020, kilingia mitaani maeneo mbalimbali ya jiji la Dar ikiwemo Buguruni, Tazara, Uwanja wa Taifa, Temeke Wailes na maeneo mengine kwa ajili ya kuzungumza na wasomaji  na kuwahamasisha kushiriki bahati nasibu hiyo dakika za lala-salama.

Wasomaji wa Tazara wakipata elimu.

Wasomaji walikutana na kikosi hicho na walihamasika na kuonekana kuyachangamkia magazeti hayo na kujaza kuponi inayoelekeza jinsi ya kushiriki shindano hilo.

Anthony Adam akiwahamasisha wasomaji kujaribu bahati yao dakika za lala-salama ili kuweza kuondoka na mchuma huo.

Akizungumza na wasomaji hao, Mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji, Anthony Adam, aliwaambia wasomaji hao kuwa pamoja na mshindi wa gari hilo pia katika droo watatafutwa washindi wengine wa zawadi kama vile simu za kisasa za mkononi (smart phones) pesa taslimu na nyinginezo.

Katika kipindi hiki cha lala-salama Anthony aliwasisitiza wasomaji hao kuchana kuponi iliyopo ukurasa wa pili kwenye magazeti hayo na kumkabidhi muuza magazeti yeyote aliye karibu nao au kuzifikishwa kwenye ofisi za magazeti haya zilizopo Sinza-Mori, Dar kwa ajili ya kuweza kujishindia gari hilo.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

CORONA! Prof .Nyagori WHO “MPENI TUZO RAIS MAGUFULI”

Leave A Reply