The House of Favourite Newspapers

Wasomi Vyuo Vikuu, Wanafunzi Sekondari Kushiriki DSE Scholar Investment


WANAFUNZI wa Vyuo vya Elimu ya Juu na Shule za Sekondari Nchini wameaswa kushiriki katika Shindano la Soko la Hisa la Dar es Saalaam lijulikanalo kama DSE Scholar Investment Challenge 2017 ambalo limezinduliwa rasmi leo Machi 31, 2017 na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar, Ibrahim Mshindo.

Akizungumza katika uzinduzi huo amesema kuwa Shindano hilo linaratibiwa na kuendeshwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam kila mwaka kuanzia Aprili Mosi hadi Juni 30, alielezea kuwa kwa Mara ya kwanza Shindano la mwaka huu litashirikisha wanafunzi wa shule za sekondari katika shindano maalum la uwekezaaji kwa kupitia mfumo wa kiteknohama unaofikiwa kwa njia ya ya tovuti ya www.younginvestors.co.tz.

Kitoka kushoto ni Meneja Masoko na Mauzo katika soko la Hisa la Dar es Saam,Patrick Msusa,Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar(DSE), Ibrahim Mshindo ambaye pia ndiye alikuwa mgeni rasmi na  Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha, Dkt. Faraji Kasidi.

Wanafunzi hao watashiriki bure kupitia tovuti hiyo ama wanaweza kushiriki kupitia Application ya Smartphone ya Leverage Scholar au kupiga namba ya simu ya *150*36#.

Katika uzinduzi huo pia imetoa fursa kwa wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Cha Arusha kushiriki uzinduzi huo la uwekezaji.

Akifafanua mbele ya wanahabari, Mshindo umesema kuwa lengo la Shindano hilo ni kuwapa wanafunzi, uelewa na mazoea ya uwekezaji katika masoko ya mitaji na Dhamana.

“Lengo la DSE la kuelimisha wanafunzi linapatikana na lengo la shirika la kimataifa la  Child&Youth Finance International.

Shirika hili la kimataifa limetenga wiki hii iliyoanza Machi 27 na kuishia leo Machi 31 kuwa wiki rasmi ya  Fedha Duniani kwa mwaka 2017.”

Wiki ya Fedha Duniani imeratibiwa kwa lengo la kuwaelimisha vijana kuhusu haki zao za kijami na kiuchumi,umuhimu wa kuweka Akiba Mara kwa Mara na kujiandaa kuingia katika ulimwengu wa sasa wa kazi na ajira kwa kushiriki katika fursa mbalimbali”.

Wanafunzi wote Nchini wameombwa kushiriki kwani kupitia Shindano hilo litawaongezea uelewa juu ya masuala ya masoko ya mitaji na Dhamana.

Comments are closed.