The House of Favourite Newspapers

Wastara Aamua Kuachana na Uigizaji

0

wastara (2)Stori: Hamida Hassan, Wikienda

Dar es Salaam: Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amejipanga kuachana na uigizaji na kufanya ishu nyingine ikiwa ni pamoja na biashara ambazo ameanza kuzifanya. Akizoza na Wikienda, Wastara alisema kuwa anamalizia kazi ya uigizaji mwaka huu na mwaka unaokuja atakuwa mwingine kabisa kwani baada ya kufika nchini Msumbiji (aliko kwa sasa) amepata dili lingine zuri ambalo ataliweka wazi baada ya mipango yake  kukamilika.

“Kinacho niachisha uigizaji si biashara tu bali ni pamoja na dili nililolipata huku Msumbiji, kama litakwenda nilivyopanga, nitaliweka wazi inshallah,” alisema Wastara.

Hivi karibuni, Wastara aliripotiwa kuwa na ujauzito ambapo alikimbilia nchini Msumbiji.

Leave A Reply