Wastara Akata Tamaa

Wastara Juma.

MWANAMAMA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ametinga jijini Dodoma kuongea na Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ambaye ameahidi kumsaidia kufuatilia mkataba wake na Wachina anaodai pesa taslimu shilingi milioni 80 za Kitanzania ingawa anaonekana kukata tamaa.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Wastara alisema hivi karibuni alifanya mazungumzo na waziri huyo, lakini kwa upande wake amekata tamaa ya kupata pesa hizo kwani mkataba wake na Wachina hao wa Kampuni ya KZG aliokuwa akiwatangazia simu zao ambao umebakiza siku chache umalizike.

 

“Unajua ni siku kama 30 tu zimebaki, naona nimezikatia tamaa, ni Mungu tu atende miujiza nipate pesa hizo. Kwa sasa ninafanya biashara zangu ndogondogo hasa za losheni ambapo nawauzia sana akina mama ili kujikwamua kimaisha kwani kupambania pesa hizo naona nimekwama kabisa,” alisema Wastara ambaye amekuwa akipambana pamoja na kuwa na ulemavu.

STORI: Shamuma Awadhi, Dar

Toa comment