The House of Favourite Newspapers

Watalii 6 Waliofariki Hifadhi ya Taifa Kenya Wapatikana

Image result for hell’s gate national park

WATU sita wameripotiwa kufariki katika Hifadhi ya Kitaifa ya Hell’s Gate nchini Kenya baada ya kusombwa na maji ya mafuriko  yaliyosababishwa na mvua kubwa siku ya Jumapili,  Septemba 1 mwaka huu.

 

Shirika la wanyamapori nchini Kenya (KWS), limeifungia hifadhi hiyo baada ya tukio hilo liliwasomba watalii sita ambao ni raia wa Kenya na raia mmoja wa kigeni ambaye bado hajulikani alipo na shughuli za kumtafuta zinaendelea, imesema KWS.Image result for hell’s gate national park

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa jana Jumatatu miili  hiyo imepatikana.

Hifadhi hiyo inasifika kwa mandhari ya kupendeza ambayo pia imetokea katika filamu ya The Lion King  na  ya “Tomb Raider: The Cradle of Life” ya mwaka 2003.

 

Comments are closed.