The House of Favourite Newspapers

Watano Waongezwa Kesi ya Kutekwa Mo Dewji

 

Mfanyabiashara Mohammed Dewji.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Julai 23, 2019, imeagiza kukamatwa kwa raia wanne wa Msumbiji ambao ni Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issac Tomo, Zacarious Junior, na raia wa Afrika Kusini Phila Tshabalala, wakihusishwa na kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji, Oktoba 11, 2018.

 

Wakili wa Serikali,  Wankyo Simon,  amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa, kuiomba mahakama hiyo hati  ya kuwakamata washtakiwa hao ili kuunganishwa katika shtaka la pili na la tatu.

 

“Upelelezi bado haujakamilika tunaiomba mahakama hati ya kukamatwa washtakiwa watano ili waunganishwe katika shauri hili,” amedai Simon.

 

Hakimu Shahidi ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 6, 2019 itakapotajwa tena.

Mo alitekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Oktoba 11, 2018 wakati akifanya mazoezi katika Hoteli ya Colosseum iliyopo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, alipatikana Oktoba 20 siku tisa baadaye, katika eneo la Gymkhana baada ya kudaiwa kutelekezwa na watekaji hao.

Comments are closed.