The House of Favourite Newspapers

Wateja na Mawakala wa Airtel Money Wajishindia Mkwanja na Tesa Kimilionea

0
Meneja Chapa wa Airtel Money Gillian Rugumamu (katikati) akiongea wakati wa droo ya 11 ya Airtel Money Tesa Kimilionea ilifonyika leo jijini Dar es Salaam. Promosheni ya Tesa Kimilionea inawapa fursa wateja na mawakala wa Airtel kujishindia zawadi za pesa taslimu Tzs100, 000, Tzs1, 000,000 au promosheni kubwa ya Tzs10, 000,000 kila mwisho wa mwezi pale wanapotumia huduma yeyote ya Airtel Money. Kulia ni Meneja Mawasiliano Airtel Jennifer Mbuya na kushoto ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Joram Mtafya.

 

KAMPUNI ya Airtel Tanzania leo imechezesha droo ya 11 ya promosheni ya Airtel Money Tesa Kimilionea ambapo wateja 100 wamejishindia Tzs100,000 kila mmoja huku wengine wawili wakijishindia Tzs1,000,000 kwa kila mmoja.

 

Promosheni ya Tesa Kimilionea ni kwa ajili ya wateja pamoja na wakala wa Airtel na wanaingia kwenye droo ya kujishindia pesa taslimu Tzs100, 000, Tzs1, 000,000 au promosheni kubwa ya Tzs10, 000,000 kila mwisho wa mwezi pale wanapotumia huduma yeyote ya Airtel Money.

Leave A Reply