Watu 10 Wauawa Kwa Bomu Istanbul, Uturuki

Istanbul (3)Miili ya marehemu ikiwa chini baada ya shambulio hilo lililotokea mapema leo huko Istanbul, Uturuki.Istanbul (2)Jeshi la Polisi wakiimarisha ulinzi.Istanbul (1)Mji wa Istanbul nchini Uturuki.

Istanbul, Uturuki

WATU wapatao kumi wameuawa leo na wengine 15 kujeruhiwa baada ya mtu asiyejulikana kujilipua kwa bomu kwenye mji wa kitalii wa Istanbul nchini Uturuki.

Maofisa wa usalama nchini humo wamesema kuwa, shambulio hilo yawezekana kuwa ni la kigaidi na huenda lilipangwa na kikosi cha wapiganaji wa Islamic State (IS) .

Afisa mmoja wa polisi aliyeshuhudia tukio hilo ameviambia vyombo vya habari chini Uturuki kuwa baada ya bomu kulipuka, ghafla aliona vipande vya mwili wa binadamu vikiruka kutoka eneo ambapo bomu hilo lililipuka, hiyo inaonesha kuwa bomu lile lilikuwa la mtu kujitoa muhanaga.

 Gari la wagonjwa liliwahi eneo la tukio na kuwapeleka majeruhi wote kwenye hospitali moja iliyopo wilaya ya Sultanahmet.

Baadayea vikosi vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo waliimarisha ulinzi zaidi kwenye eneo la tukio na maeneo mengine ya mji huo ili kujilinda zaidi endapo tukio lingine kama hilo litatokea.

Matukio mengine kama hilo yametokea mwaka jana likiwemo moja ambalo zaidi ya watu 30 waliuawa mwezi Julai kwa kushambuliwa na wapiganaji wa IS mjini Suruc, karibu na mpaka wa Uturuki na Syria.

Wakati tukio lingine ni lile la kulipuka kwa mabomu mawili ya kujitoa muhanga mwezi Oktoba nje kidogo na Stesheni Kuu ya treni huko Ankara ambapo watu zaidi ya 100 waliuawa.

Loading...

Toa comment