The House of Favourite Newspapers

17 Mbaroni Wakituhumiwa Kuua, Kubaka na Kupora

0

 

POLISI mkoani Mwanza inawashikilia watuhumiwa 17 wa makosa mbalimbali yakiwemo mauaji ya familia, ubakaji, ukatili wa kijinsia, uporaji na utengenezaji wa pombe haramu aina ya gongo.

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Muliro Jumanne, alisema hatua hiyo inafuatia msako mkali uliofanywa na jeshi hilo kuanzia Januari Mosi hada Februari 16 mwaka 2021 na kufanikiwa kukamata gari aina ya Toyota Harrier namba T121 DHE ambalo limewekewa chessis na namba za usajili wa gari nyingine.

 

Vifaa vingine vilivyokamatwa ni pamoja na pikipiki 6, Luninga 10, sabufa 4, simu za mkononi 51, mitambo 7 ya kutengenezea pombe aina ya gongo, pombe lita 100, Bangi KG 100, Mirungi KG 30 na kompyuta 2.

 

 

“Kufuatia msako huo mkali wa kata kwa kata, mtaa kwa mtaa ninahakikisha tunauongozwa na intelijensia ya jinai ili kuhakikisha hatukosei mtu lakini pia tunahakikisha tunapata sapoti ya wananchi kwenye ushahidi dhidi ya watu mbalimbali waliofanya makosa hayo,” alisema Muliro.

 

Kamanda Muliro aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Bakari Hamiss (21) mkazi wa mtaa wa Mlimani B anayejihusisha na matukio ya mauaji, John Ezekiel (25) Amosi Lucas (19), Daniel Mussa (24) wakazi wa Kayenze watuhumiwa wa makosa ya ubakaji, Said Yusufu (24) Said Ramadhani (27) Hamisi Hussein (60) na Shaban Sarehe (9) wanaokabiliwa na makosa ya ubakaji.

 

 

Aidha Muliro alitoa tahadhari kwa wamiliki wa magari na madereva ambao magari yao yanadaiwa faini kutokana makosa mbalimbali ya usalama barabarani ambapo magari 510 yalikamatwa.

 

“Natoa wito, hii haitakuwa na msalie mtume, hizo faini ambazo zimetozwa kisheria baada ya wao kufanya makosa ni pesa ya serikali tusije tukalaumiana katika hili, magari yote ambayo yametozwa faini hii wao wenyewe wakalipe kabla ya msako mkali ambao umeshaanza,” alisema Muliro.

 

Na Leah Marco, Mwanza

Leave A Reply