WATU 26 Wafariki Ajali ya Lori na Hiace Mkuranga
WATU 26 wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa baada ya gari dogo (Hiace) lililokuwa likitoka Mkuranga kuelekea Kimanzichana mkoani Pwani, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba chumvi likitokea Mtwara kuelekea Dar es Salaam.
Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 25, 2018 kijiji cha Mparange Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani
Kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Kibiti, Mohamed Likwata, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba majeruhi wote wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Wakati huohuo, Rais John Magufuli amemtumia Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, rambirambi kutokana na vifo vya watu 26 vilivyotokea wilayani Mkuruganga.
Comments are closed.