Spoti Xtra Laendelea Kukimbiza Mtaani
TIMU nzima ya promosheni ya Gazeti la Spoti Xtra, leo Jumapili kama kawaida iliingia mtaani ambapo ilipofika mitaa ya Chanika nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, ikakutana na mapokezi makubwa.
Katika hali ambayo ilionyesha wazi kwamba wasomaji wamekuwa wakilifuatilia na kulisoma Gazeti la Spoti Xtra, wakazi wa eneo hilo walionekana wakiligombania, kwa kila mmoja akitaka kopi ili apate uhondo uliomo ndani.
Wafanyabiashara, wapita njia na wengineo, kwa nyakati tofauti, walionekana wakilisoma gazeti hilo ambalo hutoka kila Jumapili.
Katika promosheni hiyo, wasomaji waliendelea kujizolea zawadi za sabuni kwa kila aliyekutwa akilisoma.
Comments are closed.