The House of Favourite Newspapers

Kim Poulsen Atimuliwa Kuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars

0
Kim Poulsen ametimuliwa kama Kocha Mkuu wa Taifa Stars

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefikia makubaliano ya kumuondoa kocha wa Timu ya Taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen kwenye benchi la ufundi pamoja na wasaidizi wake.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo, imeeleza kuwa pande zote mbili zimefikia makubaliano hayo baada ya kikao cha pamoja.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Poulsen ataendelea kubaki katika timu za taifa za vijana mpaka mkataba wake utakapokamilika na kwamba kwa sasa benchi la ufundi la Taifa Stars litakuwa chini ya kocha Hanour Janza akisaidiwa na Meck Maxime huku Juma Kaseja akiteuliwa kuwa kocha wa magolikipa.

Leave A Reply