The House of Favourite Newspapers

Watu 331 wafariki dunia mkoani Mbeya kwa ajali za barabarani 2015

0

Ajali

Jumla ya watu 331 wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani mkoani Mbeya katika kipindi cha mwaka 2015 ikiwa ni ongezeka la vifo 27 ikilinganishwa na vifo 304 vilivyotokea mwaka 2014.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Ahmed Msangi amesema ongezeko hilo la vifo linaenda sambamba na ongezeko la makosa ya usalama barabarani na idadi ya wahalifu wa makosa hayo.

ajali 2

Katika mahojiano maalumu na Kituo Star TV, Kamanda Msangi amesema mwaka 2014 jumla ya makosa 61,466 yamepatikana wakati mwaka jana makosa yalikuwa 76,346 ikiwa ni ongezeko la makosa 14,898 ambapo kati yake mwaka 2015 makosa 71, 429 na 54,849 ya mwaka 2014 kwa pamoja yametozwa adhabu zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 3 na Milioni 203 ikiwa ni ongezeko la Shilingi Milioni 497.4 kwa tozo za mwaka 2014.

Kuhusu Pikipiki za miguu miwili na mitatu maarufu kama na Bajaji, Kamanda Msangi amesema ajali zake nazo zimeongezeka kutoka 141 mwaka 2014 mpaka 159 mwaka jana ambazo kwa pamoja zimesababisha vifo 162 na kujeruhi watu 231 na kwamba nyingi zimesababishwa na uzembe wa kukosa umakini kwa madereva.

Jiji la Mbeya lina pikipiki za miguu mitatu zaidi ya 2100 wakati pikipiki za miguu miwili ni zaidi ya 3000.

Leave A Reply