The House of Favourite Newspapers

Watu 36 Wafariki kwa Mafuriko

0

SHIRIKA la Uokoaji la Msalaba Mwekundu nchini Uganda linaloendelea na uokoaji katika Wilaya ya Bundibugyo, limesema kuwa watu wengi bado hawajulikani walipo kutokana na mvua kubwa zinazonyesha Mashariki mwa Uganda.

Waziri wa Kujikinga na Majanga na Kushughulikia Wakimbizi, Musa Echweru, amesema takriban kaunti ndogo 11 zimesombwa na mafuriko na uokoaji unakuwa mgumu kutokana na miundombinu kuharibiwa vibaya.

Mikoa ya Bugisu na Bundibugyo karibu na Mlima Ruwenzori imeathiriwa vibaya zaidi huku mafuriko na maporomoko ya udongo yakiwaacha maelfu ya watu bila makazi na wakilazimika kujisitiri katika shule au makanisa.

Aidha, Echweru ameongeza kuwa sehemu zilizoathiriwa zipo katika hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko na yanayosambazwa kwa maji, na serikali imesema imetoa fedha za dharura kwa ajili ya kupambana na magonjwa, chakula na kurekebisha miundombinu.

Leave A Reply