The House of Favourite Newspapers

Watu 43 walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa na moto ulioteketeza jengo la ghorofa saba

0

Watu 43 walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa na moto ulioteketeza jengo la ghorofa saba katika kitongoji cha mji mkuu wa Bangladesh Alhamisi, maafisa walisema.

“Watu 43 walifariki kutokana na moto,” waziri wa afya wa Bangladesh Samanta Lal Sen aliiambia AFP baada ya kuitembelea hospitali ya mjini Dhaka ya Medical College Hospital.

Inspekta mkuu wa polisi Bacchu Mia alisema mtu mwingine alifariki kwenye hospitali ya polisi ya mjini Dhaka na kuongeza idadi ya vifo kuwa 44.

Afisa wa idara ya zimamoto Mohammad Shihab alisema moto huo ulianzia katika mgahawa maarufu wa biriyani kwenye barabara ya Bailey mjini Dhaka Alhamisi usiku na kusambaa haraka hadi kwenye ghorofa za juu, na kufanya watu wengi wakwame.

Leave A Reply