The House of Favourite Newspapers

Watu 55 Wauawa Katika Mapigano ya Polisi na Mgambo wa Kikabila Uganda

ugandan_police
WATU wasiopungua 55 wameuawa leo katika mapigano makali yaliyotokea magharibi mwa Uganda kati ya majeshi ya usalama na mgambo wa mfalme mmoja wa kikabila.

Msemaji wa Polisi, Andrew Felix Kaweesi, alisema polisi 14 na mgambo 41 wamekufa katika mapigano kwenye mji wa Kasese jana (Jumamosi) wakati wapiganaji wa ufalme wa Rwenzururu walipowashambulia polisi waliokuwa katika doria.

“Jana, taarifa ya pamoja ya oparesheni ya Jeshi la Polisi la Uganda na Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) ilisema kwamba majeshi hayo yakiwa katika doria yalishambuliwa na majeshi ya ulinzi ya mfalme huyo ambapo yalirusha bomu la mkono lililotengenezwa kienyeji  na kumjeruhi askari mmoja.

Hivyo, majeshi ya usalama yalirusha risasi katika kujihami na kuwaua washambuliaji wanne,” alisema Kaweesi akiongeza kwamba tukio hilo liliibua mapigano yaliyoendelea tangu asubuhi hadi jioni.

Msemaji huyo aliongeza kwamba washambuliaji hao ambao wote hawakuwa kutoka kikosi cha walinzi wa mfalme huyo, walikuwa na bunduki, mikuki na mabomu yaliyotengenezwa kienyeji.

halotel-strip-1-1

Christian Bella Azungumzia Standup Comedy na Studio Yake Mpya

Comments are closed.