Watu 63 Wafariki Bomu Likilipuka Harusini

WATU wapatao 63 wameuawa na wengine 182 kujeruhiwa baada mtu asiyefahamika, aliyekuwa na bomu kujitoa mhanga, jana Jumapili Agosti 18, 2019,  katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul,  wakati watu hao walipokuwa wakihudhuria sherehe ya harusi.

 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya ndani, Nasrat Rahimi, alisema kuwa shambulio hilo limetokea magharibi mwa mji wa Kabul kwenye idadi ndogo ya Washia, katika ukumbi wa harusi uliokuwa umejaa watu waliokuwa wakisherehekea.

 

Rahimi alisema kwamba miongoni mwa waathirika ni wanawake na watoto. Shambulio hilo limetokea huku kundi la Taliban pamoja na serikali ya Marekani wakijadili namba ambayo taifa hilo kubwa duniani litaondoa vikosi vyake vya kijeshi nchini Afghanistan kwa lengo la kutafuta amani.
Hata hivyo, kundi la Taliban limekana kuhusika na shambulio hilo.


Loading...

Toa comment