The House of Favourite Newspapers

Watu Laki 4 Watoroka Mlipuko wa Volkano Congo

0

UMOJA wa Mataifa umesema kwamba zaidi ya watu 400,000 wametoroka Mji wa Goma nchini DR Congo kutokana na hofu ya kuzuka kwa mlipuko mwengine wa Volkano karibu na mto Nyiragongo.

 

Jana Alhamisi, maofisa waliagiza watu waondoke katika mji huo, kwa madai kwamba lava ya Volkano inayoingia ziwa Kivu inaweza kusababisha tsunami na wingu la gesi ya sumu hali iliyosababisha nusu ya mji huo kubaki mahame.

 

Kuondoka huko kwa watu hao kulisababishwa na kuongezeka kwa matetemeko ya ardhiyaliokuwa yakitoka katika Mlima Nyarigongo na hofu huenda ukalipuka tena.

 

Aidha, Mji wa Sake umefurika watu na sasa wanaelekea nchi jirani ya Rwanda, hifadhi ya wanyamapori ya Virunga na hata Ziwa Kivu. Mashirika yá misaada yameanza kutoa msaada huku watu walioachwa bila makao wakitafuta chakula na maji.

 

Mitetemeko ilikuwa michachesiku ya Alhamisi usiku hali iliosababisha wengine kuwa na matumaini kwamba hali huenda ikawa shwari. Lakini sauti kadhaa zimekuwa zikisikikakutoka kwa mlima huo.

Leave A Reply