The House of Favourite Newspapers

Watuhumiwa Wa Ubakaji, Udhalilishaji Wapandishwa Kizimbani Moro

0

Moro

Watuhumiwa wa ubakaji Zuberi Thabit (wa kwanza kushoto) na Idd Adamu (wa pili kushoto) wakielekea kizimbani leo.

 

wabakaji (3)

Watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi.

wabakaji (1)

Safari ya kuelekea kizimbani ikiwa imeiva.

  Wabakaji Moro (1)

Waandishi wa habari wakiwasubiri watuhumiwa wapande kwenye difenda.

Wabakaji Moro (2)

Watuhimiwa wa ubakaji Ramadhani Ally (26) ambaye ni mkazi wa Dakawa aliyedaiwa kuwa kinara wa kusambaza video za tukio hilo (mbele), Zuberi Thabit anayetuhumiwa kwa ubakaji (katikati) na Idd Adamu (wa kwanza kushoto) anayetuhumiwa kwa kurekodi video za ubakaji wakitoka mahabusu kuelekea mahakamani.

Wabakaji Moro (3)

Ramadhani Ally akipanda difenda.

Wabakaji Moro (4)

Watuhumiwa wa ubakaji wakiwa ndani ya difenda kuelekea mahakamani.

Wabakaji Moro (5)

Safari ya kuelekea mahakamani ndani ya difenda.

Wabakaji Moro (6)

Idd Adamu ndani ya difenda.

Wabakaji Moro (7)

Wanahabari wakichukua picha za watuhumiwa.

Wabakaji Moro (8)

Ndugu wa Ramadhani (msambazaji wa video) wakiangua vilio baada ya kumuona ndugu yao akishuka kwenye difenda.

Wabakaji Moro (9)

Zuberi Thabit mtuhumiwa wa ubakaji.

Wabakaji Moro (10)

Idd Adamu mtuhumiwa wa kurekodi video za ubakaji.

Na Danstan Shekidele, Morogoro
WATUHUMIWA Zuberi Thabit mkazi wa Mbalizi mkoani Mbeya na Idd Adamu, mkazi wa Iringa, leo wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumbaka na kumdhalilisha mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa) wa Dakawa mkoani Morogoro, tukio linalodaiwa kufanywa wiki mbili zilizopita katika nyumba moja ya kulala wageni.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Morogoro, maofisa wa mahakama hiyo waliwaambia waandishi wa habari kuwa kesi hiyo itasikilizwa faragha ili kutoa nafasi kwa watu wote kutamka maneno na kuona vielelezo bila hofu, hivyo hawataruhusiwa kusikiliza.

Kesi hiyo inayosikilizwa na hakimu Mary Moyo imevuta hisia za wakazi wengi wa mjini hapa, hasa baada ya tukio hilo kusambaa kwa kasi kubwa katika mitandao ya kijamii na simu za mikononi.

Awali, ilidaiwa kuwa Zuberi Thabit ambaye ndiye mtuhumiwa wa ubakaji, ni dereva wa trekta aliyeenda huko Dakawa kwa ajili ya kazi za kilimo, sawa na Idd Adam na akiwa huko, ndiko alimpata mwanamke huyo na kumfanya kuwa patna wake.

Baada ya kumaliza mkataba, inadaiwa Thabit alimtaka mpenzi wake huyo kwenda nyumba moja ya kulala wageni kwa lengo la kuagana, lakini wakiwa wanafanya mapenzi, ghafla alijitokeza Idd ambaye alikuwa uvunguni, aliyeibuka na kuanza kuwarekodi.

Inadaiwa kwamba baada ya kumaliza ‘recording’ hiyo, wanaume hao walitimka zao, lakini wiki mbili baadaye, wakawatumia video marafiki zao wa Dakawa, wakiwa na lengo la kuwadhihaki kwa kumdhalilisha dada yao.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

 

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply