The House of Favourite Newspapers

Watumiaji wa Airtel Money Wajizolea Milioni Kila Mmoja, Wengine 100 Waondoka na Laki Kila Mmoja

0
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kulia) akizungumza kwenye hafla ya uchezeshaji wa droo hiyo, kushoto ni msimamizo kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga na katikati ni Meneja wa Chapa ya Aitel Tanzania Gillian Rugumamu.

 

 

KAMPUNI ya Mtandao wa Simu ya Airtel kupitia ambayo inaendelea na promosheni yake ya Tesa Kimilionea ambapo wateja wake wanaotumia huduma yake ya Airtel Money wanajishindia zawadi mbalimbali ikiwemo magari pesa taslimu leo imechezesha droo ya sita ya promosheni hiyo na kuwapata washindi 102.

Katika droo iliyotawaliwa furaha na nderemo kutoka kwa washindi waliokuwa wakipigiwa simu baada ya namba zao kuibuka na ushindi katika droo hiyo washindi hao 100 waliibuka na laki moja kila mmoja na washindi wawili wenye bahati zaidi waliibuka na kitita cha shilingi milioni moja kila mmoja.

Wachezeshaji wa droo hiyo wakionesha nyuso za furaha baada ya mmoja wa washindi kupatikana.

 

 

Akizungumza wakati wa uchezeshwaji wa droo hiyo Meneja Uhusiano wa Aitel Tanzania, Jackson Mmbando amesema jinsi ya kushiriki promosheni hiyo ni kutumia huduma za Airtel Money ambapo unachotakiwa ni kubonyeza *150*60# kufanya miamala mbalimbali.

 

Mmbando ameongeza kuwa promosheni ambayo inawahusu pamoja na mawakala wa huduma ya Aitel Money popote walipo hapa nchini inaendelea na kuwataka wateja wa Airtel kuendelea kutumia huduma hiyo.

Droo hiyo ilichezeshwa na Aitel chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha hapa nchini. HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply