The House of Favourite Newspapers

Watumishi Sita Missenyi Matatani Kwa Ubadhirifu, Majaliwa Atoa Tamko – Video

0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza watumishi sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi wafuatiliwe ili warejeshe fedha za umma na kisha wachukuliwe hatua za kinidhamu.

“Uongozi wa Mkoa uendelee kuwafuatilia na kuisimamia Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ili warudishe fedha za makusanyo za Julai na Agosti, 2023.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo jioni (Jumamosi, Septemba 23, 2023) wakati akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa katika tarafa ya Bunazi, wilayani Missenyi, mkoani Kagera.

Leave A Reply