The House of Favourite Newspapers

Watumishi wa Sekta Binafsi Nao Kucheka Kabla ya Julai – Mwenyekiti TUGHE

0
Joel Kaminyoge, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Taifa

MWENYEKITI wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Taifa bwana Joel Kaminyoge amesema watumishi wa sekta binafsi watarajie kucheka wakati wowote kabla ya tarehe moja mwezi wa saba kutokana na bodi ya kima cha chini cha mishahara kwa sekta binafsi kuelekea mwishoni mwa ukamilishaji wa zoezi la upangaji wa mishahara.

 

Kaminyoge amebainisha hayo mkoani Njombe alipokuwa kwenye ziara yake ya kawaida ya kuimarisha Chama alipokutana na watumishi ambao ni wanachama wa chama hicho katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Njombe.

Watumishi wa Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe

“Upandishwaji wa mishahara umefanywa kwenye sekta ya umma,wakati wowote kabla ya tarehe moja july watumishi kutoka sekta binafsi na wenyewe watacheka na hii ni kwasababu kuna bodi mbili za kima cha chini cha mshahara,hii sekta ya umma imeshafanya ndio maana Rais ametangangaza hii sekta binafsi bado wanaendelea kufanya wakati wowote tutasheherekea kwa pamoja”alisema Joel Kaminyoge

Leave A Reply