The House of Favourite Newspapers

Wauza Jezi Feki za Yanga Wanaswa Dar

0

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limewakamata watu 17 kwa tuhuma za kuuza jezi bandia za timu ya Yanga Afrika 1,208 zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya GSM.

Kazi hiyo ilifanyika katika maeneo mbali mbali ya Jiji Dar es salaam, lakini pia kwa kushirikiana na baadhi ya mikoa nchini kwa kipindi cha kuanzia tarehe Januari 2 hadi Januari 28, 2022.

Kamanda wa Polisi Kanda Malalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema katika Jiji la Dar es salaam Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa watano, akiwemo Zahiri Hassan (17) aliyekutwa Uwanja Benjamin William Mkapa akiwa na Jezi bandia za timu ya Yanga seti 52.

Wengine ni Majiba Ndahya (50) ambaye alikamatwa maeneo ya Kariakoo mtaa wa Agrey akiwa na Jezi seti 124, Mohamed Ramadhani alikutwa na Jezi seti 86, John Staslaus alikamatwa na Jezi seti 39 na Emmanuel Kinasa alikutwa na Jezi seti 60.

“Watuhumiwa hao waliwataja wenzao wa Zanzibar, ambapo Uwanja wa Amani watuhumiwa watatu walikutwa na Jezi bandia seti 36, Jezi zingine bandia 134 zilipatikana kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Tanga na Mwanza ambapo watuhumiwa tisa walikutwa na Jezi seti 811.

Aidha Kamanda Muliro amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawatahadharisha wananchi wote wanaojihusisha na vitendo vya kutengeneza, kuuza na kusambaza, bidhaa kwa kuiga au kufananisha nembo za biashara au huduma za watu wengine iliyosajiliwa kisheria, kufanya hivyo ni kosa na kinyume na sheria za nchi.

“Jeshi la Polisi litashirikiana na mamlaka nyingine za kisheria ili kuona watuhumiwa wamechukuliwa hatua kali za kisheria,” amesema Kamanda Muliro.

Leave A Reply