The House of Favourite Newspapers

Zuchu: Diamond ni Romantic

0


WAKATI KUKIWA na tetesi mitandaoni kwamba huenda Msanii kutoka lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othman ‘Zuchu’ akavishwa pete siku ya wapendanao na bosi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz,’ Zuchu amefunguka rasmi kuwa Platnumz ni romantic.

Zuchu amemuelezea Diamond wakati wa interview na kituo cha television cha Wasafi kwamba kiongozi huyo ambaye amewahi kuwa kwenye mahusiano kadha na Mastaa kama Wema Sepetu, Zarinah Hassan, Hamisa Mobeto, ​​na Tanasha Donna kuwa ‘Platnumz’ ni “romantic, anajitoa na anjari mpenzi wake.”

Alipoulizwa kuhusu Hamisa, Zari na Tanasha ikiwa kuna mmoja ana mkubali zaidi na angependa kuwa na Diamond, Zuchu alisita na hakutaka kutoa maelezo ingawa alikubali ushauri kwamba Diamond inafaa abaki na Zuhura na kufunga naye ndoa.

Leave A Reply