The House of Favourite Newspapers

Wawa Azuia Mabadiliko ya Okwi Taifa

Mshambuliaji Emmanuel Okwi.

 

BEKI wa kati ya Simba, Pascal Wawa, jana alimzuia kocha wa timu hiyo, Patrick Aussems, asifanye mabadiliko baada ya mshambuliaji Emmanuel Okwi kuumia. Okwi aliumia dakika ya 69, baada ya kudondoka wakati akiwania mpira na beki wa Al Ahly na kutolewa uwanjani kwa machela.

 

Mara baada ya mshambuliaji huyo kutolewa nje na machela, Aussems alimtuma kiongozi mmoja wa benchi la ufundi kwenda kumuita mchezaji ili aingie, lakini Wawa alikimbia haraka na kumzuia kocha huyo kufanya mabadiliko.

Wawa ambaye jana alionyesha kiwango cha juu alikwenda kwa kocha huyo na kuzungumza naye kwa sekunde chache huku akinyoosha kidole kwa Okwi aliyekuwa akitibiwa na mwisho kocha huyo aligoma kufanya mabadiliko. Hata hivyo, dakika moja baadaye Okwi alirejesha uwanjani na kuendelea na mechi hiyo.

Stori na Ibrahim mussa, Dar es Salaam

 

Comments are closed.