The House of Favourite Newspapers

Iringa: Wazee wa Kimila Waiangushia Maombi Bombardier – Video

WAKATI wa Mkoa wa IRINGA jana, Aprili 29, 2019, walipokea ndege ya kwanza ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Dash 8 Q400, baada ya kutua katika uwanja wao, mapokezi ya ndege hiyo yaliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Ally Hapi, wananchi pamoja na wazee wa kimila wa mkoa huo.

 

Katika mahojiano, wazee hao wamemmwagia sifa Rais Dkt. John Magufuli na kumshukuru kwa kutekeleza ahadi zake na kwamba ndege hiyo wameiona ni nzuri sana.

 

Aidha, wazee hao walifanya maombi maalumu kwa Rais Magufuli, Mkuu wa Mkoa, Ally Hapi pamoja na ndege za hiyo ya AIR TANZANIA.

TAZAMA TUKIO HILO

Comments are closed.