The House of Favourite Newspapers

Wazee wa Kimila SUMBAWANGA Wamfanyia Tambiko Diamond – Video

Diamond Platnumz

 

STAA wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama ‘Diamond Platnumz’ amefanyiwa tambiko la ulinzi na wazee wa kimila wa Mji wa Sumbawanga, mkoani Rukwa ambako amekwenda kwa ajili ya Tamasha la Wasafi Festiva.
Diamond amefayiwa tambiko hilo leo Jumamosi, Desemba 8, 2018 na wazee wa Mtaa wa Senti katika Kata ya Kizwite mara baada ya kumaliza kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule katika mtaa huo.
Diamond Platnumz’ akifanyiwa tambiko la ulinzi na wazee wa kimila wa Mji wa Sumbawanga, mkoani Rukwa
Akimfanyia tambiko hilo, mmoja wa wazee wa Kimila katika eneo hilo alimtaka Diamond kukaa kwenye kiti cha kimila kisha kuanza kumsemea maneno; “Tumefurahi sana kututembelea hapa leo na kuweka jiwe la msingi la shule yetu, ninakuomba ukalie hiki kiti (anampa kiti), hata ukifika nyumbani kwako umetoka kwenye mihangaiko, usikalie kochi, kalia hiki kiti ndiyo utamaduni na mila zetu.
“Japo una ulinzi, lakini pokea hii silaha kwa ajili ya kukulinda (anampa upinde na mshale), huu ni ulinzi wa kiutamaduni, hii ni bunduki na risasi vitakulinda nyumbani kwako, tunawashukuru wewe na ugeni wote uliyokuja nao hapa.
Aidha, Diamond amewashukuru wazee hao na wananchi wa mtaa wa Senti kwa kukabidhiwa ulinzi huo, ambapo pia shule hiyo imeitwa jina la Diamond.
PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL

VIDEO: TAZAMA TUKI HILO HAPA

Comments are closed.