The House of Favourite Newspapers

Waziri Ajiuzulu kwa Kuvunja Masharti ya Corona

0

WAZIRI wa Afya wa Uingereza, Matt Hancock   Juni 28, amejiuzulu wadhifa wake  baada ya kuvunja Sheria ya kuweka umbali wa mtu mmoja hadi mwingine (Social Distance)  akiwa na Msaidizi wake Mkuu, Gina Coladangelo anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

 

Picha za Waziri huyo zilizochapishwa katika Gazeti la The Sun zilimuonesha Hancock na Coladangelo wakibusiana katika ofisi moja ya Wizara hiyo ya Afya.

 

Katika barua yake ya kujiuzulu aliyoiandika kwa Waziri Mkuu, Boris Johnson, Hancock alisema anataka kusisitiza ombi lake la msamaha kwa kuvunja muongozo na kuiomba radhi familia

 

Waziri Mkuu Boris Johnson amesema amesikitishwa mara baada ya kupokea barua ya kujiuzulu kwa Waziri huyo wa afya.

Leave A Reply