The House of Favourite Newspapers

Waziri Alitaka Shirika la Posta Kwenda Kidijitali

Kuandikwa akisoma hotuba yake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Luteni Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, akizungumza katika hafla hiyo.
Kaimu Posta-Masta Mkuu, Hassan Mwang’ombe, akisoma hotuba yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Elias Kuandikwa, akizindua nembo mpya.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya magari yaliyotolewa na Umoja wa Posta Duniani (UPU).

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Elias Kuandikwa, amelitaka Shirika la Posta nchini kufanya kazi kwa bidii na kwenda kidijitali ili kurahisisha utendaji wake na hivyo kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli.

Kuandikwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipozindua nembo mpya itakayokuwa ikitumiwa na shirika hilo ambapo pia amelipongeza kwa namna lilivyojizatiti kufanya kazi kwa nguvu.

Wakati huohuo, akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Posta-Masta Mkuu, Hassan Mwang’ombe, amesema uzinduzi wa nembo hiyo mpya una maana kubwa kwani ni moja ya mikakati ya menejimenti ya shirika hilo likiungwa mkono na bodi ya wakurugenzi.

Nembo tunayotumia sasa ambayo mwisho wake ni leo, ilianza kutumika tangu Januari 1994 wakati Shirika la Posta lilipoanzishwa,” alisema Mwang’ombe.

Aidha amesema mabadiliko hayo ya nembo yanaenda sambamba na kubadili muundo wa shirika katika utendaji kazi wake na kuanzishwa kwa kampuni mpya nne zenye lengo la kuimarisha kiuchumi shirika hilo, ambazo ni: PostaGiro FinancialService (Posta Microfinance); Posta Logistics Company Ltd; Posta freight & forwarding; na Posta digital company.

Vilevile, katika hafla hiyo magari manne yamezinduliwa ambayo yalitolewa na mfuko unaosimamiwa na Umoja wa Posta Duniani (UPU) kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na shirika hilo kiutendaji.

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.