The House of Favourite Newspapers

Waziri Ashatu Kijaji Akabidhi Tuzo Kwa Gf Trucks & Equipment’s Ltd Mkoani Geita

0
Waziri wa Viwanda na uwekezaji, Ashatu Kijaji akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa kwanza kwa makampuni yanayouza na kusambaza Magari na mitambo Migodini Afisa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Gf Trucks & Equipments Ltd, Poul Msuku wakati wa kufunga maonyesho ya Madini mkoani Geita.

Kampuni ya uuzaji na uunganishaji wa magari na mitambo ya Gf Trucks & Equipment’s Ltd imebuka kampuni ya kwanza inayouza na kusambaza Magari na mitambo ukanda wa mikoa ya kanda  ya ziwa.

Hayo yamejiidhirisha wakati wa kufunga  maonyesho ya 5 ya teknolojia ya madini mkoani Geita na kuibuka kampuni bora ya usambazaji na uuzaji wa mitambo.

Waziri wa viwanda na uwekezaji Ashatu Kijaji akimkabidhi funguo ya mtambo wa kuchimbia Madini (Excavator ) ya XCMG Mkurugenzi wa kampuni ya G Unity ,Ezekiel Rembo baada ya kununua katika maonyesho ya madini kwa punguzo malum mkoani Geita.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na  Waziri wa Viwanda na uwekezaji,  Ashatu Kijaji  Afisa masoko na mauzo wa kampuni ya GF Poul Msuku alisema wanafurahia kuibuka washindi katika kipengere hicho na wanachukua tuzo hiyo kama chachu ya kujipanga na kuongeza nguvu kaitia uwekezaji kwa kanda ya ziwa

Gf Trucks ambao ni wauzaji wa mitambo na mashine za migodini aina ya XCMG, na magari ya kubebea mizigo ya FAW na Hongyang  tuna wateja wengi wanaojiusisha na Uchimbaji wa madini na shudhuli za usafirishaji nchini
Pia Gf waliitumia siku ya kufunga maonyesho kwa kukabidhi  Mtambo wa kuchimbia madini kwa mteja aliyenunua katika maonyesho hayo ya madini kwa bei ya punguzo.

Mkurugenzi wa E Unity akiangalia mtambo wa Excavator baada ya kukabidhiwa katika viwanja vya maonyesho.

Pia Waziri Kijaji aliwataka Gf kuwekeza zaidi katika kwawezesha wachimbaji wadogowadogo ili waweze kujikomboa na kwa kuwawekea utaratibu rahisi  kumudu gharama  ikiwemo mikopo rahisi  na pia aliwataka wachimbaji hao kuchapa kazi itakayoweza kumwongezea kipato na kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi.

Naye Mkuurugenzi wa kampuni ya G Unity  Squre Ltd, Ezekiel Rembo aliwashukuru GF kwani kwa kushiriki katika maonysho hayo wameweza kununua mashine hiyo (XCMG) kwa gharama nafuu tofauti kama wangeifata Dar essalaam na ameokoa zaidi ya shilling million 10 ikiwamo gharama ya mafuta kuitoa Dar hadi Geita alimaliza .

Leave A Reply