The House of Favourite Newspapers

Mwigulu Awaponda Wabunge Waliokimbia Kisa Corona

0

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, amesema kitendo cha baadhi ya wabunge wa upinzani kususia vikao vya Bunge kwa kuogopa Corona ni ishara ya kutengeneza madaraja na mpango wa kushusha uchumi wa nchi.

 

Amesema hayo jana Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Viwanda na Biashara ya makadirio na matumizi kwa mwaka wa fedha, 2020/2021 ambapo amewataka Watanzania kuacha kusikiliza miluzi ambayo inapotosha taifa.

 

“Maisha ya Watanzania mara nyingi hayana akiba, hivyo kitendo cha  kujifungia ndani bila kufanya kazi kwa tahadhari ya Corona kama wanavyoshauri baadhi ya wabunge wa upinzani panaweza kutengeneza majanga mengine, hivyo wanatakiwa kufuata ushauri uliotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuchapa kazi na kuondoa hofu juu ya Corona na kubainisha kuwa janga halikimbiwi,” alisema.

 

Nchemba aliteuliwa na Rais  Magufuli hivi karibuni kuiongoza Wizara ya Katiba na Sheria, tukio lililofanyika Mjini Chato mkoani Geita baada ya aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Dkt. Balozi Augustine Mahiga kufariki dunia.

Na Faustine Gimu, Dodoma

 

Leave A Reply