The House of Favourite Newspapers

Waziri Dk.Ndumbaro Atoa Agizo Kwa Taasisi Zake Kushirikia Tamasha La Majimaji Selebuka

0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameziagiza Taasisi zote za Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zinatangaza Utalii na zinafanya Uhifadhi kuweza kushiriki Tamasha la Majimaji Selebuka.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma kuanzia tarehe 24 Julai hadi 31 mwaka huu katika Uwanja wa Majimaji Songea likiwa na lengo la kuhamasisha utalii wa ndani, michezo pamoja na kukuza na kuenzi utamaduni wetu.

Ametoa agizo hilo wakati akizindua msimu wa saba la Tamasha hilo uliofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia 24 na 25 Aprili katika Viwanja vya Makumbusho ya Majimaji ikiwa ni maandalizi ya Tamasha lenyewe litakalofanyika mwezi Julai kwa muda wa siku saba mkoani hapo

Katika Tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu limebeba kauli mbiu isemayo ” Misitu ni Uchumi ” Dkt.Ndumbaro amesema kwa mwaka huu Tamasha linatoa hamasa kwa Jamii kutunza misitu zaidi.

Waziri Dkt. Ndumbaro amesema anategemea Tamasha hilo kwa mwaka huu litakuwa kubwa sana na litatoa fursa kwa Watu mbalimbali kuanza kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii ambavyo vipo mkoani Ruvuma likiwemo Pori la Akiba Lipalamba

Katika hatua nyingine, Amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Songea kutumia mamlaka yake ya kuzitaka Taasisi zilizo katika wilaya yake kushiriki katika Tamasha hilo.

” Mkuu wa wilaya najua una Taasisi nyingi sana katika wilaya yako ninakuomba na ninaamini una Mamlaka hiyo, toa maelekzo kwa Taasisi zote zinanazotoa huduma na kufanya biashara zishiriki Tamasha la Majimaji Selebuka ” alisisitiza Waziri Dkt.Ndumbaro

Aidha amezitaka Halmashauri ya Songea pamoja Halmashauri zingine ziweze kushiriki Tamasha hilo
Aidha, Waziri Dkt. Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuziomba Taasisi nyingine za Watu binafsi kushiriki katika Tamasha hilo ili ziweze kutoa huduma kwa jamii katika msimu wa Tamasha hilo.

Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo Reinfrida Rwezaura, amesema Tamasha hilo tangu kuanzishwa kwake limekuwa ni Jukwaa bora kwa kuwakutanisha Wafanyabiashara, Wajasiliamali, wanamichezo, wanafunzi, na wadau mbalimbali katika kuendelea kuutangaza uchumi na utalii nchini

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameziagiza Taasisi zote za Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zinatangaza Utalii na zinafanya Uhifadhi kuweza kushiriki Tamasha la Majimaji Selebuka.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma kuanzia tarehe 24 Julai hadi 31 mwaka huu katika Uwanja wa Majimaji Songea likiwa na lengo la kuhamasisha utalii wa ndani, michezo pamoja na kukuza na kuenzi utamaduni wetu.

Ametoa agizo hilo wakati akizindua msimu wa saba la Tamasha hilo uliofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia 24 na 25 Aprili katika Viwanja vya Makumbusho ya Majimaji ikiwa ni maandalizi ya Tamasha lenyewe litakalofanyika mwezi Julai kwa muda wa siku saba mkoani hapo

Katika Tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu limebeba kauli mbiu isemayo ” Misitu ni Uchumi ” Dkt.Ndumbaro amesema kwa mwaka huu Tamasha linatoa hamasa kwa Jamii kutunza misitu zaidi.
Waziri Dkt. Ndumbaro amesema anategemea Tamasha hilo kwa mwaka huu litakuwa kubwa sana na litatoa fursa kwa Watu mbalimbali kuanza kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii ambavyo vipo mkoani Ruvuma likiwemo Pori la Akiba Lipalamba

Katika hatua nyingine, Amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Songea kutumia mamlaka yake ya kuzitaka Taasisi zilizo katika wilaya yake kushiriki katika Tamasha hilo.

‘” Mkuu wa wilaya najua una Taasisi nyingi sana katika wilaya yako ninakuomba na ninaamini una Mamlaka hiyo, toa maelekzo kwa Taasisi zote zinanazotoa huduma na kufanya biashara zishiriki Tamasha la Majimaji Selebuka ” alisisitiza Waziri Dkt.Ndumbaro

Aidha amezitaka Halmashauri ya Songea pamoja Halmashauri zingine ziweze kushiriki Tamasha hilo
Aidha, Waziri Dkt. Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuziomba Taasisi nyingine za Watu binafsi kushiriki katika Tamasha hilo ili ziweze kutoa huduma kwa jamii katika msimu wa Tamasha hilo.

Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo Reinfrida Rwezaura, amesema Tamasha hilo tangu kuanzishwa kwake limekuwa ni Jukwaa bora kwa kuwakutanisha Wafanyabiashara, Wajasiliamali, wanamichezo, wanafunzi, na wadau mbalimbali katika kuendelea kuutangaza uchumi na utalii nchini.

Leave A Reply