The House of Favourite Newspapers

Kigwangalla Azindua Mashindano ya Golf ya NCBA Jijini Arusha

0
Meneja wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa Benki ya NCBA, Bw Gift Shoko akishiriki katika mashindano ya NCBA Golf Tournament yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Arusha kama sehemu ya uzinduzi wa matawi mapya ya benki hiyo katika mkoa wa Arusha.                                              
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizindua rasmi mashindano ya NCBA Golf Tournament yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Arusha. Mashindano hayo yaliyokuwa sehemu ya uzinduzi wa matawi mapya ya benki ya NCBA jijini Arusha yalilenga kukuza sekta ya utalii na ukuaji wa biashara.
Wadau mbali mbali wa michezo na biashara wakijadiliana jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) wakati wa uzinduzi wa mashindano ya NCBA Golf Tournament yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana Arusha. Mashindano hayo yaliyokuwa sehemu ya uzinduzi wa matawi mapya ya benki ya NCBA jijini Arusha yalilenga kukuza sekta ya utalii na ukuaji wa biashara nchini.
Leave A Reply