The House of Favourite Newspapers

Waziri Mhagama Aipongeza WCF Kwa Kuwapatia Computer Tume Ya Usuluhishi

0

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kuipatia vitendea kazi (computers) Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ili kuharakisha shughuli za usuluhishi wa migogoro ya kikazi.

 

Pongezi hizo zimetolewa na Mhe. Waziri Jenista wakati akikabidhi computer 10 kwa Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Bw.Shanes Nungu katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mfumo wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Mbeya Novemba 29, 2021.

“Tunashuhudia hapa Workers Compensation Fund (Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi) unakwenda kufanya kazi nzuri ya kuiwezesha CMA ili itekeleze majukumu yake sawasawa jambo hili ni zuri sana.” Alifafanua Mhe. Waziri.

 

Kipekee napenda kuwashukuru sana sana wakuu wote na viongozi wa taasisi zote Dkt. John Mduma Mkurugenzi Mkuu wa WCF na kaka yangu Nungu Mkurugenzi Mkuu wa CMA kwa kuona umuhimu wa kufanya kazi kama serikali moja, ninyi wote mko chini ya umbrella (mwamvuli) mmoja, ili kuhakikisha kwamba mmoja anapogundua changamoto ya mwenzake anaamua kusimama naye na kuweza kumsaidia, Alisisitiza Mhe. Waziri Jenista Mhagama

 

Akieleza zaidi, Mhe. Waziri alisema Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa ukifanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yake tangu uanzishwe miaka sita iliyopita, sheria iliyokuwepo kabla ya kupata uhuru, mfanyakazi alikuwa akiumia analipwa shilingi 108,000/= haijalishi awe amepata ulemavu wa aina gani malipo ya fidia yalikuwa ni flat rate.

“Mwaka 2008 Sheria ilifanyiwa marekebisho ambapo mwaka 2015 tuliunda Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ambao umechukua jukumu la Fidia, kuhangaika na magonjwa na madhara yatokanayo na kazi kutoka kwa waajiri na kuwekwa kwenye Mfumo maalum na sasa uko kwenye Mfuko wa WCF.” Alibainisha.

 

Alisema katika muktadha huo huo wa kuhakikisha serikali inayagawa majukumu kiutendaji na kisheria ilianzisha CMA ili taasisi hii ishughulike na masuala ya usuluhishi na uamuzi inapotekea migogoro ndani ya maeneo ya kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma alisema, makabidhiano hayo ya computer ni utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama aliyetaka taasisi hizo zifanye kazi kama ndugu.

 

“Kwa kufanya kazi kwa pamoja ndipo tunaweza kufikia malengo yetu kama taasisi lakini kwa pamoja kama ofisi yako Mheshimiwa Waziri, tunatambua kwamba mmoja wetu kama atakimbia mbio na uwezo wake alionao na akawaacha ndugu zake nyuma “hatatoboa yeye peke yake”. Alisema Dkt. Mduma.

 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Bw. Shanes Nungu alimshukuru Waziri Jenista kwa maono yake na kuwezesha CMA kupata msada huo wa computer.

“Mheshimiwa Waziri nakumbuka ulisema nyie watoto sita kwanza shikamaneni halafu saidianeni na agizo lako limezaa matunda, sio mara ya kwanza kwa WCF kutusaidia mara ya kwanza walitusaidia computer kumi ambazo zilisaidia kutatua malalamiko ya wananchi kucheleweshewa hukumu zao kupungua.” Alishukuru Bw. Nungu.

 

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge) Bw. Kspar Muya, wakurugenzi wa WCFna CMA pamoja na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo ni NSSF, PSSSF, OSHA na Idara ya kazi.

Habari @imeldamtema

Leave A Reply