The House of Favourite Newspapers

Chid Beenz Aachia Album Yake Mpya

0
Album mpya ya rapa Chid Beenz inayokwenda kwa jina la W2 WANGU imetoka rasmi na sasa inapatikana kupitia majukwaa mbalimbali ya ku-stream muziki mtandaoni.
 
Album ya WA2 WANGU yenye jumla ya nyimbo 18, ina kolabo 5 pekee, Chidi akiwapa mashavu wasanii kama Baddest, Brian Simba na wengineo kusikika kwenye album hiyo.
 
Hata hivyo, Chidi tayari alishaachia nyimbo 6 toka kwenye album hiyo, ambazo ni Nahamia Bar, Jirani, Walete, One, King of the Jungle na hilo ngoma.
 
Rapa Chidi Beenz ambaye ni mshindi mara nne Kill Music Awards kupitia tuzo ya msanii Bora wa Hip Hop nchini, album yake hii mpya (Watu Wangu) inaifuata album ya “Dsm Stand Up” ambayo ndio album yake ya kwanza kuiachia kwenye muziki wake, ilitoka mwaka 2010.
Leave A Reply