The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Akifanya Usafi Eneo la Coco Beach – Video

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo ameungana na wakazi wa wilaya ya Kinondoni kufanya usafi katika eneo la ufukwe wa Coco Jijini Dar es Salaam na kutoa wito kwa manispaa hiyo kuboresha maeneo ya kutolea huduma ili yaendane na hadhi ya fukwe hiyo.

 

Akizungumza mara baada ya kufanya usafi na kupanda mti katika eneo hilo waziri Mkuu ameitaka halmashauri ya manispaa ya Kinondoni kuhakikisha wanaboresha vibanda vya watoa huduma za vyakula, ulinzi na mandhari ya eneo hilo ili liwe kivutio zaidi kwa wananchi wanaolutumia. I

 

“Eneo hili la Coco Beach nimelitembelea bado haliridhishi kwa usafi, nimeenda kwenye fukwe pale nimekuta takataka nyingi zimelundikwa mahali, na wakati mwingine pia tumeona wafanyabiashara wa mihogo zile takataka nazo wanaenda kuzitupa baharini” amesema Lugola.

 

Majaliwa ambaye ameambatana na Mke wake Mama Marry Majaliwa akaelezea maamuzi yaliyofikiwa kuhusiana na fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya mashujaa hapa nchini.

 

Awali akimkaribisha waziri Mkuu, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Happi ameelezea mipango mbalimbali ya kuboresha ufukwe wa Coco na kuahidi kusimamia usafi katika eneo hilo.

 

Tanzania huadhimisha siku ya mashujaa wake waliopoteza maisha katika harakati za kuipigania nchi ifikapo Julai 25 ya kila mwaka.

Waziri Mkuu Akifanya Usafi Eneo la Coco Beach – Video

Comments are closed.