The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Ashauri Hospitali zinazotibu Saratani kuwa na Wodi Maalum

0
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa (kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin P. Mhede (katikati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam  East Africa, Julius Magabe (wa pili kushoto) wakimkabidhi mfano wa hudi ya milioni 100 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru (kushoto), fedha zilizopatikana kwenye NMB Bima Marathon kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto wenze ugonjwa wa saratani Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin P. Mhede (wa pili kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam East Africa, Julius Magabe (kushoto) wakimkabidhi mfano wa hudi ya milioni 100 Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa (katikati). Fedha hiyo zilizopatikana kwenye NMB Bima Marathon zimetolewa kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto wenze ugonjwa wa saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akimshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa tatu kulia) mara baada za kupokea hundi hizo. Wa pili kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa pamoja na meya kuu wakishuhudia.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin P. Mhede (wa pili kushoto), pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa NMB Bima Marathon.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akionesha mfano wa hudi hizo juu mara baada za kukabidhiwa.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin P. Mhede (wa pili kushoto), pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa NMB Bima Marathon.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin P. Mhede (wa pili kushoto), pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa NMB Bima Marathon.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) akizungumza katika NMB Bima Marathon.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (katikati) akishiriki mazoezi ya viungo pamoja na maofisa wengine waandamiyi toka NMB na washiriki wengine wa NMB Bima Marathon.
Baadhi za washiriki wa NMB Bima Marathon wakivishwa medali mara baada za kumaliya mbio zao.
Picha za pamoja ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa meza kuu pamoja na wadau wa NMB Bima Marathon
Picha za pamoja ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa meza kuu pamoja na washindi mbalimbali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (katikati). Katikati zao ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji) Angellah Kairuki pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge (kulia).

Kulia mwalimu wa mazoezi za viungo akiongoza mazoezi ya viungo kwa washiriki wa NMB Bima Marathon.

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameziagiza hospitali zote za rufaa ambazo zinatoa matibabu ya ugonjwa wa saratani kwa watoto kuangalia uwezekano wa kuwa na wodi maalum kwa ajili ya wagonjwa hao.

 

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea mfano wa hudi ya shilingi milioni 100 zilizochangwa na wakimbiaji wa NMB Bima Marathon, fedha zilizotolewa kwa ajili ya kusaidia matibabu ya ugonjwa wa saratani kwa watoto kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.

 

Akikabidhi hundi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin P. Mhede, pamoja naye  Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ambao ni waratibu wa mbio hizo, alisema wameguswa na kundi hilo la wagonjwa wa saratani ambao wanaitaji msaada hivyo kuamua kuwasaidia kwa kiasi kilichopatikana.

 

Baada za Waziri Mkuu Majaliwa kukabidhiwa hundi hizo, alimkabidhi rasmi moja kwa moja Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru ambapo alieleza kuwa gharama kubwa za matibabu za ugonjwa wa saratani imekuwa kikwayo kwa jamii hivyo wanafarijika michango na misaada inazotolewa kusaidia matibabu hazo.

 

Mbio za NMB Bima Marathon zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam zilishirikisha wakimbiaji mbalimbali wa kuanzia kilomita 5, 10, 20 ambapo zimekuwa na muitikio mkubwa wa washiriki kutoka makampuni anuai, ambapo washindi walikabidhiwa medali na fedha.

Leave A Reply