The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Waziri Mkuu atajwa Bungeni

0

BREAKING-NEWS1majaliwa

Waziri Mkuu Mteule Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa.

Rais Dk. John Pombe Magufuli amemteua Majaliwa Kassim Majaliwa, Mbunge wa Ruangwa  kuwa Waziri Mkuu wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jina lake limetajwa bungeni muda huu.

Mhe. Majaliwa atathibitishwa kwa kupigiwa kura na wabunge wote muda mfupi ujao.

Kassim Majaliwa

Kassim Majaliwa alizaliwa Desemba 22, 1960 na ana umri wa miaka 54.

Ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

WASIFU WAKE:

Elimu
Toka Hadi Jina la Shule/Chuo Cheti
1970 1976 Mnacho Primary School Cheti cha Elimu ya Msingi
1977 1980 Kigonsera Secondary School CSEE
1991 1993 Mtwara Teachers College
1994 1998 University of Dar es Salaam Bachelor Degree
1999 1999 Storckolm University PGDP
Uzoefu
Toka Hadi Jina la Mwajiri Ngazi/Wazifa
2010 2014 MB
2006 2010 PM Mkuu wa Wilaya
2001 2006 PS-CWJ Katibu Mkoa
2001 2001 PS-CWJ Katibu Wilaya
1988 2000 PS-Moec Mkufunzi
1984 1986 TD-Lindi Council Mwalimu
Burudani
  •   Soka
Leave A Reply